Archive pour janvier, 2015

CIBITOKE:ZAIDI YA WATU 120 WAUAWA.

5 janvier, 2015

IMG_20150105_020436Mapigano makali yaliozuka siku 5 zilizopita huko Cibitoke kati ya jeshi la taifa na wale wanaoshukiwa kuwa waasi kutoka Congo tayari yameshasababisha vifo vya watu 117, wengi wao wakiwa ni waasi hao ambao wengine waliuwa kwa mapanga hata baada ya kujisalimisha.

Kwa jumla, waasi 105 wameuwawa huku jeshi la taifa likipoteza askari 12. Pia vifaa vya kivita vilikamatwa ikiwa ni moja wapo na zana tano za kurusha mabomu, bunduki zaidi ya mia moja na vinginevyo.

Kwa upande wake, viongozi serikalini wametaja kuwa zoezi hilo ni la muhimu sana na limetiwa msisitizo ili kutoa funzo na kwa wengine wenye nia kama hiyo, na kuwaonyesha kuwa Burundi haina nafasi tena ya kuikaribisha vita kutokana na mengi iliyopitia.

Ama kwa mujibu wa upizani na mashirika ya kutetea haki za binaadamu kama APRODH, wanalaani vitendo na tabia za jeshi katika kupambana na janga hili. Hasa, wanakemea matumizi mabaya ya raia kwa kuwashirikisha moja kwa moja katika mapigano na kuwauwa bila huruma waasi ambao hukamatwa bila hata kuheshimu sheria na haki za kibinaadamu.

Ni wazi kwamba hali hii inaleta wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia, ikiwa imesalia miezi michache tu ili uchaguzi mkuu kufanyika nchini Burundi. Hakika, hatma ya nchi kwa sasa ipo mikononi mwetu sote, ikiwa raia, viongozi serikalini, wapinzani, mashirika mbalimbali,  kila mmoja wetu, kadri na uwezo wake, anastahili kushugulishwa na hali halisi ya nchi yetu, kutafakari na kuchukua hatua mbadala ili kuepuka machafuko kama ya miaka iliyopita.

Kwa hili, tunatakiwa kuweka tofauti zetu pembeni na kushikamana. Kuzua vurugu huchukua mda mdogo ila kuizima na kurejesha hali ya kawaida huchukua mda mrefu sana. Burundi kwa sasa, ni sawa na mtu aliefanya ajali na kupooza viungo vyote vya mwili, baada ya matibabu ya muda mrefu, sasa ameanza kutambaa, unafkiri mtu huyo atakua katika hali gani akikumbwa na ajali tena? Hata iwe ndogo kiasi gani, ni wazi kwamba itamuathiri kwa kiwango kikubwa mno.

BAKARI Ubena

 

NKURUNZIZA s’adresse au peuple pour le nouvel an / Hotuba ya rais.

2 janvier, 2015

IMG-20150101-WA0030Dans un discours adressé à la nation à l’occasion du nouvel an, à partir de Ngozi, au nord du pays, sa province natale,le président burundais, Pierre Nkurunziza, a notamment  demandé, mercredi soir, à la Commission électorale nationale indépendante (Ceni) d’être impartiale.

Tout en remerciant tous ceux qui ont aidé pour que l’opération d’enrôlement des électeurs s’opère dans la paix et la sécurité,  le président de la République a apprécié la bonne volonté de  la Ceni  pour la bonne attitude qu’ils ont manifestée en rencontrant les représentants des parties prenantes aux élections en vue d’analyser avec eux les irrégularités constatées au cours de l’enrôlement des électeurs. Et cela dans le but  de trouver des solutions pour l’intérêt de tous.

Il a également apprécié la décision d’accorder une opportunité à ceux qui n’ont pas pu s’inscrire : « Ce qui fera que tout le monde, sans exclusion ou auto-exclusion, participera aux élections. Nous les invitons à continuer sur cette voie, et à trouver des mécanismes crédibles de faire le suivi, gérer et corriger les irrégularités observées », a-t-il insisté

« Les élections se dérouleront merveilleusement bien », a-t-il rassuré précisant que les Burundais en sont habitués. Et de déclarer : «  qu’il s’agisse de quelqu’un qui voudrait  rester au pouvoir ou y accéder, tout le monde le sait, il n’y a aucune autre voie  si ce n’est la voie des urnes. »

Il appelé les politiciens à accepter « la compétition politique sans animosité » et à « respecter et faire respecter la décision du peuple : le verdict des urnes ».

Aux corps de défense et de sécurité, il a demandé  d’agir par une bonne conduite durant la période électorale  et  dire ‘’ non ‘’ aux sollicitations  politiciennes:A la Communauté Internationale, il  a  enfin demandé d’envoyer sans délais les observateurs de ce processus électoral et de décaisser les fonds promis à cette fin.

Selon le calendrier électoral, l’élection des députés et des conseillers communaux est prévue le 26 mai 2015.

KISWAHILI:

Katika hotuba hiyo aliyoitoa mkoani Ngozi alipozaliwa, rais wa jamhuri, Pierre Nkurunziza aliiomba pia kamati huru  ya taifa ya uchaguzi kuwa waadilifu. Aliwashukuru pia walio changia ili kukosoa baadhi ya mambo yalikwenda kinyume kama uandikishwaji wa wapiga kura. Aliipongeza CENI pia kwa kufanyz kila waliwezalo kwa manufaa ya wote.

Nkurunziza alisisitiza pia kuwa uchaguzi utaendeshwa vizuri bila matatizo yoyote, huku akitaja kuwa Warundi wanao uzoefu huo. Kakumbusha pia kuwa, kwa kila anaetaka kubaki ao kuingia madarakani hakunz njia nyengine ispokuwa uchaguzi pekee. Alitoa wito pia kwa wanasiasa wenza, kukubali ushindani bila ya unyama wowote huku akiwataka pia kuheshimu maamuzi ya raia na kuheshimu na kuheshimisha kura zao.

Aliwataka pia wenye kulinda usalama wafanye kazi yao vema na wasiitike wito wowote wa kisiasa na akiwataka jumuiya ya kimataifa kuwatuma haraka iwezekanavyo wasimamizi wa chaguzi hizo na kutoa pesa walizoahidi katika mchakato huo. Ikumbukwe kuwa, kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi, uchaguzi wa madiwani na wabunge unatarajiwa kufanyika May 25 mwaka huu wa 2015.

BAKARI Ubena.