Archive pour mars, 2015

Unamfahamu Bi Aziza Kulsum GULAMALI?

30 mars, 2015

shenila mwanza gulamaliNi mwenye asili ya hindia na pakistani kupitia wazazi wake, lakini Aziza Kulsum GULAMALI alizaliwa nchini BURUNDI mwaka 1944.Ni mfanyabiashara mashuhuri na anaefahamika zaidi katika ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika Mashariki kwa ujumla. Licha ya kushtumiwa kwa kipindi kirefu kuhusika na biashara za magendo za sigara kupitia kiwanda chake UZABUTO, alitajirika pia kupitia biashara ya madini ya COLTAN na dhahabu. Alitajwa pia katika mzunguuko wa usambazaji haramu wa silaha huku akishtumiwa kutoa msaada mkubwa kwa chama FDD cha Burundi, kipindi hicho kikiwa maguguni.

Kwa jina maarufu ‘MAMA GULAMAL’, ni mfanyabiashara mashuhuri na mtu muhimu hasa katika nchi za BURUNDI, RWANDA na RDCongo ambapo baada ya vita ya pili nchini humo mnamo 1998, yeye aliekuwa rafiki wa wahutu, aliamuwa ghafla kujiunga na watutsi na akawa mshirika mkuu wa FPR chama tawala nchini Rwanda, na kufaanikiwa kuchukuwa uongozi  mkuu wa SOMIGL (Société Minière des Grands Lacs) na kuwa mfanyabiashara wa pekee wa COLTAN huko KIVU ya Kusini.

Licha ya kuwa mfanyabiashara mashuhuri, Bi Aziza alijua pia kusoma na kuendana na hali halisi ya sehemu aliyotaka kuendesha biashara zake. Alijua kujenga hali ya maelewano na kundi la siasa ao la kijeshi lenye uwezo na nguvu sehemu hiyo ili biashara zake zisikutane na vikwazo. Licha ya hayo, aliwahi pia kuishi nchini Ubelgiji ambapokwa kipindi kadhaa alizidi kuandamwa na kesi za magendo ya madini ya Coltan na uuzaji haramu wa silaha.

Taarifa za hivi karibuni zilibainisha kuwa Mama GULAMAL alikuwa na Akaunti 3 katika benki HSBC-Private BankUnamfahamu Bi Aziza Kulsum GULAMALI? dans Liens arrow-10x10 ya huku nchini USWISI tangu mwaka 1995. Akaunti mbili miongoni mwa hizo zilifungwa mnamo kipindi cha mwaka 1997-2000. Mwaka 2007, iliripotiwa kuwa moja mwa akaunti zilizofungwa ilikuwa na kiwango cha pesa Milioni 3.26 za Dollar za Kimarekani.Bi Aziza hakulalamikia hilo na wala hakutoa taarifa yoyote. Hii ikiwa ni moja mwa sababu zilizomfanya kurudi kuishi Afrika.

Itakumbukwa kuwa, Bi Aziza Kulsum, kupitia vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa kama RFI, alikanusha kabisa tuhuma hizo dhidi yake hasa kuhusu kuhusishwa kwake katika biashara haramu ya silaha na madini ya Coltan huku akisisitiza kuwa jina la GULAMAL halipo katika vitambulisho vyake. Bi Aziza ana mtoto wa kikeajulikanae kwa jina la SHENILA MWANZA (pichani hapo juu), ambae ni seneta nchini RDC kupitia chama RPDC katika ukanda wa FIZI.

Kwa sasa Bi Aziza Kulsum ‘GULAMAL’, inasemekana makaazi yake makuu ni nchini Congo huko BUKAVU na mara kadhaa huingia na kutoka mjini BUJUMBURA.

« Haki zote zimehifadhiwa »—-  April-2015

BAKARI Ubena.-