Archive pour avril, 2015

Maandamano makali yaanza mjini Bujumbura.

26 avril, 2015

Baada ya hiyo jana chama tawala kumtangaza Pierre Nkurunziza kuwa ndie mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa juni mwaka huu, tayari hali ya vurugu imeanza kutanda kote nchini baada ya raia kuandamana vikali mabarabarani kwa kuzuzia mabarabara kwa kuchoma ma tairi na hata wengine kupambana na askari polisi.

IMG-20150426-WA0006

 

Milio ya risasi inarindima kote nchini hususan mjini Bujumbura. Wilaya za Nyakabiga, Cibitoke na hasa Musaga ndipo kunaporipotiwa vurugu zaidi za waandamanaji hao ambao wameitikia kwa wingi wito wa upinzani na hata wengine wakidhihiridha kuchoshwa na utawala wa Cndd Fdd na hasa ule wa Pierre Nkurunziza. Tayari majeruhi wameanza kuhesabika kwa wingi huku hali ikizidi kuwa tete.

IMG-20150426-WA0007

 

Mapema leo asubuhi, mpinzani mkuu wa chama FNL Agathon Rwasa alitangaza wazi kupinga hatua hiyo ya rais mstaafu kutaka kuwania muhula wa tatu ambao ni kinyume na katiba ya nchi na mkataba wa Arusha. Aliendelea kwa kusema kuwa, uamuzi huo bila shaka utairudisha nchi ya Burundi katika machafuko mabaya zaidi baada ya kupata amani na usalama.

Ikumbukwe kuwa Umoja wa Ulaya na Marekani wanapinga waziwazi uamuzi huo na ndio maana hawakuitikia wito kunako kongamano la chama tawala hiyo jana. Aliskika raia akiongea « Niwakumbushe tu kuwa chama tawala kiliingia madarakani kwa mtuto na bila shaka ni hivo tu ndio njia ya kuwang’atua madarakani. Laa sivyo tukubali kuongozwa na madikteta mpaka watakapoishiwa nguvu na uwezo. »

IMG-20150426-WA0001

 

Tunaendelea kufuatilia hali halisi na kukujuzeni kwa kina zaidi. Alamsiki. MOLA INUSURU BURUNDI.

BAKARI Ubena

NKURUNZIZA na KAGAME , UNAFIKI MTUPU!

15 avril, 2015

Screenshot_2015-04-15-10-08-36-1

 

Habari wapenzi wasomaji wa bujadiaspora. Ni matumaini yangu kuwa nyote mpo salama na hiyo ndio furaha kwangu. Nitanguze shukrani za dhati kwa Muumba kwa kuniamsha salama siku ya leo na kunipa afya tele. Wengi miongoni mwetu hawakuipata bahati hii, ni wajibu kwetu kushukuru na kuitumia vema siku hii ili iweze kutufaa leo duniani ima na kesho akhera.

Wengi mlifahamu kuwa mnamo tarehe 13/04/2015, marais wawili jirani, yule wa Rwanda Paul Kagame na wa Burundi Pierre Nkurunziza walikutana huko HUYE ambayo zamani iliitwa Butare kwa mazungumzo ya kisiasa baina ya mataifa haya mawili ambayo bila shaka hali ya maelewano ilikuwa si shwari siku za hivi karibuni kutokana na tuhma mbalimbali kati ya mataifa haya.

Hali hiyo ya mfarakano ilisababishwa na matokeo kadhaa kama kukutwa kwa maiti katika mto mpakani huku nchi hizi mbili wakitupiana lawama kwa kuhusika na tukio hilo, mapigano yaliopita huko Cibitoke na kadhalika. Baada ya hapo, Rais Nkurunziza alionyesha wazi kutaka kukutana na rais Kagame bila mafaanikio. Rais huyo wa Rwanda alionyesha wazi dharau yake na kukataa wito huo.

Rais Nkurunziza alipopata habari kuwa Kagame anatarajia kufanya ziara yake huko Huye ili kutembelea chuo kikuu kilichopo sehemu hiyo, ndipo alipokurupuka na kuacha shughuli zake huko Ngozi alipokuwepo na kujielekeza huko kukutana na Kagame.

Kinachohuzunisha zaidi ni madhumuni ya ziara hiyo. Maombi yote aliyokuja nayo rais Nkurunziza ilikuwa wazi kuwa Kagame hangeliweza kuyapatia suluhu ao hata kuweza kumpa msaada wake ispokuwa kumkejeli na kumfanya kama kikaragosi na kivutio cha watu. Miongoni mwa maolbk hayo ni pamoja na :

-1.Kuwaruhusu wakimbizi wote warundi walioko Rwanda kurejea makwao.

-2.Kuomba ruhsa ya kuwasaka na hatimae kuwarudisha Burundi wapinzani wake kama Hussein Radjabu na Alexis Sinduhije walioko Kigali na kadhalika…

Bila shaka hii inaonyesha ni jinsi gani rais Nkurunziza anatapatapa bila ya kujua kipi afanye. Inaonyesha wazi upungufu wake wa uelewa katika siasa ya nchi yake na ile ya ukanda unaomzunguuka. Kamwe Kagame hawezi kuruhusu wakimbizi kurejea Burundi ikiwa walichokimbia hakijatafutiwa suluhu ya kudumu. Nchi ya Rwanda ambayo ilikutana na mauwaji ya kimbari (genocide) mwaka 1994, yaliyoendeshwa na wahutu dhidi ya watusi, haiwezi kumsaidia mhutu wa jirani nae atende kosa hilohilo. Siasa si kuvaa tu makoti bali ni kuifahamu historia na pia kusoma alama za nyakati ulizomo ili kustahwisha sera zako. Hili Nkurunziza halifahamu nadhani.

Ikiwa Nkurunziza atang’ang’ania kutaka kubaki madarakani kimabavu, basi hili ni hatari sana kwake maana jumuiya ya kimataifa ileshatangaza wazi kuwa haitoruhusu kosa lililofanyika Rwanda kujitokeza tena katika ukanda huu wa maziwa makuu. Na ndio maana kamwe Rwanda haitowafurusha wakimbizi ao wapinzani wa serikali ya sasa ya Burundi. Hili ni kwa manufaa ya wote. Ikibidi ikiwa bado hayajaanza, Rwanda ipo tayari kumsaidia mpinzani yeyote (Rajabu ao Sinduhije) ilimradi tu atawale badala ya wanaotaka vurugu na hatimae amani na usalama vidumu.

Intabwirwa ibwigwa nuko amaso atukuye… Nkurunziza aelewe wazi kuwa, uhai wake yeye mtu mmoja ni bora upotee ili kuokoa maelfu ya raia wasio na hatia. Na hili halitoshindikana endapo atazidi kuwa jeuri na kukataa ushauri. Nimkumbushe kidogo tu, kama alivowahi kusema mwenyewe, atakae anzisha vurugu, itaanzia na kuishia kwake mwenyewe. Msemo huu hata naye pia unamhusu…. Alamsiki.

BAKARI Ubena

@All rights reserved/2015.be

 

 

India yaamuru raia wake kuondoka Burundi haraka iwezekanavyo.

9 avril, 2015

Screenshot_2015-04-09-17-52-15

Ikiwa imesalia miezi kadhaa tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Burundi, hali ya usalama imeendelea kuwa ya kutatanisha kote nchini. Ripoti mbalimbali zimearifu wananchi kuihama nchi kwa kukimbilia nchi jirani ya Rwanda, Tanzania na hata Congo. Vitendo vya kinyama vyaendelea kuripotiwa kote nchini huku vijana wenye silaha wa chama tawala « Imbonerakure » wakiwa mstari wa mbele kutekeleza vitendo hivyo kwa raia na hata wanasiasa.

Baada ya balozi mbalimbali nchini Burundi kutoa wito kwa raia wake kuwa makini na kuepuka mikusanyiko ya watu na kuzurura usiku, sasa ni zamu ya nchi ya India kuwaamuru raia wake wote kuondoka nchini Burundi haraka iwezekanavyo yaani kabla ya tarehe 15 April 2015.

Wiki kadhaa zilizopita, balozi wa Ufaransa na ule wa Ubelgiji walitoa tangazo rasmi kwa raia wao kuwa makini wanapokuwa katika mizunguuko yao mjini Bujumbura na kote nchini na pia kuepuka mikusanyiko ya watu endapo kutakuwa na maandamano ya aina yoyote.

Wananchi wote wapo katika hali ya wasiwasi wakihofia machafuko kujitokeza endapo rais Pierre Nkurunziza atatangaza rasmi kuwa mgombea wakati ambapo sheria ya nchi (katiba) na makubaliano ya Arusha hayamruhusu tena. Baraza la Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Marekani wameshatangaza rasmi msimamo wao wa kupinga nia hiyo.

Fununu zinaripoti kuwa kuna uwezekano ya kwamba hiyo kesho rais Nkurunziza akatangaza rasmi nia yake na kuwa mikakati mbalimbali imeshaandaliwa ili kukabiliana na wananchi watakaoshuka mabarabarani. Idara ya upelelezi na viongozi kadhaa wa kiusalama waliokaribu na ikulu wako tayari kwa lolote. Majina ya Kazungu na Nyamitwe yametajwa sana katika mipango hiyo.

Mola Inusuru Burundi. Mola Ibariki Burundi.

BAKARI Ubena.-